Bella na Kloe ni mapacha wanaopendana sana na hufanya kila kitu pamoja. Lakini siku moja, janga linatokea pale ambapo Bella anachomeka na sufuria ya supu inayochemka. Kwa sababu ya majeraha makubwa ya moto katika maeneo kadhaa ya mwili wake, analazimika kulazwa hospitalini kwa miezi kadhaa ili kupata matibabu na baadaye anafanyiwe upasuaji wa kupunguza makovu. Hadithi hii ya picha kwa watoto ni simulizi kuhusu mshtuko na kupona. Inasimulia ajali hiyo, athari zake kwa jinsi Bella anavyojiona, uhusiano wake na dada yake pamoja na familia nzima, na umuhimu wa familia, msaada, na upendo wakati wa kupona kwake.